Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki (EHLA-DER), Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Qadir Akaras, katika khutba ya Swala ya Idi ya Adh-ha huku akisisitiza dhana ya “Hijra”, “Muqawama” na “Umoja wa Umma wa Kiislamu”, alisema kwamba; wito wa “Allahu Akbar” ndiyo silaha kubwa zaidi dhidi ya ubeberu na Uzayuni.
Qadir Akaras, rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki, aliongoza Swala ya Idi ya Adh-ha katika Msikiti wa “Kawthar Ahlul-Bayt”.
Katika khutba yake ya Idi, akirejelea vipengele vya kiroho na vya ndani vya ibada za Hijja na kuchinja, alisisitiza umuhimu wa kupambana na dhulma katika ulimwengu wa Kiislamu, kuunga mkono safu ya muqawama na umuhimu wa kujenga ustaarabu wa Kiislamu mbele ya ubeberu wa kimataifa.
Akaras akieleza kwamba: Hijja na kuchinja ni alama ya hijra ya mwanadamu kutoka katika “nyumba ya kidunia” iliyojengwa na nafsi, matamanio na dhulma kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, alisema kuwa; ibada hii si tu kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine, aliongeza: “Mwanadamu anayehama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hujitenga hata na mavazi yake, na huacha nyuma kila kilicho cha kupita ili aelekee kwa Mwenyezi Mungu wa Milele, kama vile Nabii Ibrahim alivyomwacha mkewe na mwanawe katika jangwa kavu, kila kutengana na hijra ndani yake kuna mafungamano ya kuungana na ukweli wa milele.”
Rais wa huyo katika sehemu nyingine ya hotuba yake alisema kwamba; dhana ya “Allahu Akbar” ni kubwa zaidi kuliko kaulimbiu ya kawaida, na akasisitiza kuwa ibara hiyo ina maana ya kukataa nguvu zote za kidunia, ubeberu na utawala wa kimataifa.
Alisema: “Allahu Akbar maana yake ni kuingia katika ufalme wa Mwenyezi Mungu aliye juu ya kila maelezo, tukisema Mungu ni mkubwa kuliko Marekani, tutakuwa hatujaelewa kikamilifu maana ya Allahu Akbar, Tunaposema Allahu Akbar, kwa hakika tunakiri kwamba hakuna nguvu yenye uhalisia wa kweli isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Allahu Akbar" si kaulimbiu ya wakati wa ushindi au maandamano pekee; bali maana yake ni kuweza kusema: mauti kwa Marekani na mauti kwa Israel.”
Akaras pia huku akilinganisha kujisalimisha kwa Nabii Ibrahim katika kumtoa mwanawe sadaka na kujitoa mhanga Imam Hussein (as) huko Karbala, alirejelea muqawama wa wananchi wa Ghaza na Lebanon na kusema: “Leo huko Ghaza na Lebanon, baba na mama ambao usiku wanawaangalia watoto wao kwa matumaini, asubuhi wanakutana na miili yao iliyokatwakatwa vipande vipande, wajibu wetu ni mzito; lazima tuunganishe ujumbe wa Karbala na safu ya muqawama na tuchukue hatua kwa ajili ya mwamko wa Umma wa Kiislamu na ubinadamu.”
Mwisho wa khutba yake, rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki, huku akirejelea jinai za Uzayuni na ubeberu wa kimataifa, aliitaja imani kuwa ndiyo silaha muhimu zaidi ya safu ya muqawama, na akahuisha kumbukumbu za mashahidi wa muqawama tangu operesheni ya “Tufan al-Aqsa”.
Pia katika hafla hiyo, palisomwa dua maalumu kwa ajili ya roho za mashahidi wa muqawama, miongoni mwao ni Imam Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Sayyid Hassan Nasrullah, Ismail Haniyya na Yahya Sinwar, na dua zikafanywa kwa ajili ya majeruhi wa safu ya muqawama.
Maoni yako